KARIBU

Tuesday, February 14, 2012

Mtoto wa sumari ataka kumrithi baba yake

MBIO za kuwania ubunge wa Arumeru Mashariki zimeanza na tayari jana wananchama wawili wa CCM walijitokeza kuchukua fomu kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Edson Lihweuli amewataja waliochukua fomu zilizoanza kutolewa jana kuwa ni Williamu Sarakikya (38) na Sioi
Sumari.
Kwa mujibu wa Lihweuli, Sarakikya ambaye ni mkazi wa Nkoaranga ndiye aliyekuwa mwanachama wa kwanza kuchukua fomu hiyo na kufuatiwa na Sioi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Akheri. Sioi ni mtoto wa kwanza wa marehemu Sumari; mbunge aliyepita aliyepita katika Jimbo hilo la Arumeru Mashariki.
Tambo za wagombea
Mara baada ya kuchukua fomu, Sarakikya alisema katika uchaguzi uliopita alikosa nafasi hiyo ya kuteuliwa kwa kuwa alikuwa mgenikatika siasa. Sarakikya alisema katika muda huo alijifunza mengi kuhusu siasa na sasa amejipanga kikamilifu kuwania nafasi hiyo na hatafanya makosa.
Naye Sioi alisema amechukua fomu za kuwania ubunge, ili ashiriki kupunguza ama kumaliza changamoto zilizopo ndani ya jimbo hilo. Sumari alisema yeye ni mkazi wa jimbo hilo na ameshatembelea matawi yote na kujua changamoto hizo ila kwa sasa hawezi kuzitaja mpaka muda ukifika atazitaja na namna gani atashirikiana na wana CCM na wasio wana CCM kuzipatia ufumbuzi.
Mgombea wa CCM
Wakati huo huo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyomaliza kikao chake Dodoma juzi, imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa chama hicho atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo ya NEC iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, mgombea wa chama hicho atatangazwa rasmi Februari 27, mwaka huu na Kamati Kuu ya chama hicho.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema jana kuwa mwisho wa kuzirudisha fomu zilizoanza kutolewa jana ni Februari18, mwaka huu. Alisema Februari 20,mwaka huu Mkutano Mkuu wa jimbo hilo utaitishwa ili kupiga kura za maoni, tofauti na ilivyozoeleka kura hizo kupigwa kwenye matawi.
“Mabadiliko haya ni kwa uchaguzi huu mdogo tu kwa sababu hatuna muda wa kuzunguka kwenye matawi yetu yote ya jimbo hilo,” alisema Nape. Alisema Februari 21, mwaka huu Kamati ya Siasa ya Wilaya itajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Februari 24 mwaka huu Kamati hiyo ya mkoa itajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya CCM.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 27 mwaka huu Kamati Kuu ya chamahicho itateua na kumtangaza rasmi mgombea wa chama hicho katika jimbo hilo. Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jeremeih Sumari kufariki dunia mapema mwezi uliopita kwa ugonjwa wa saratani ya ubongo.
Uchaguzi wa madiwani
NEC pia ilitoa ratiba ya uchaguzi wa madiwani katika kata nane za Tanzania Bara ambazo pia wanachama walianza kuchukua fomu jana lakini mwisho wa kuzirejesha utakuwa Februari 16, mwaka huu. Nape alisema kuanzia Februari 17 hadi 21, mwaka huu itakuwa ni muda wa kampeni za uchaguzi kwenye matawi hayo na Februari 22 kutafanyika mikutano mikuu ya matawi ya kupiga kura za maoni.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 25 mwaka huu kamati za siasa za wilaya zitajadili wagomea na kutoa mapendekezo yao kwa kamati za siasa za mikoa ambazo nazo zitawajadili wagombea hao na kutoa mapendekezo Februari 27 na halmashauri kuu za mikoa zitateua wagombea Februari 29, mwaka huu.
Taarifa zingine NEC
Pamoja na hayo, Nape alisema NEC pia ilipokea maelezo kutoka serikalini kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa madaktari nchini na mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya. “Wajumbe wameitaka Serikali kuhakikisha inachukua hatua haraka za kumaliza kabisa mgogoro huo ili usirejee tena na kuitaka ijijengee utamaduni wa kumaliza migogoro kama hiyo mapema kabla ya kuleta madhara makubwa kwa wananchi,” alisema.
Alisema mkutano huo pia ulijadili suala la chama hicho kuanzisha Kamati ya Maadili ambapo mjadala mkali uliibuka wa kutaka ama kamati hiyo iingizwe kwenye katibaya chama hicho au la.
Alisema katika kukamilisha mambo zaidi ya 20 ya mabadiliko ya chama hicho ikiwemo kujivua gamba, tayariwameanza kupata mafanikio hasa katika eneo la kutaka chama hicho kujiendesha chenyewe bila kutegema ruzuku. Kwa sasa kwa mujibu wa Nape, mikoa mitatu ikwemo Mwanza, Arusha na Dar es Salaam inajiendesha yenyewe

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Facebook Themes