KARIBU

Thursday, February 2, 2012

Fomu za big brother zatoka

Fomu za ushiriki wa shindano la BIG BROTHER AFRICA zimetoka leo, ambapo tayari mpaka saa tano asubuhi watanzania zaidi ya 15 walikua tayari wamejitokeza kuchukua hizo fomu ambazo zinatolewa bure.
haya ni baadhi ya maswali yaliyopo kwenye fomu.
historia yako, lugha ya nyumbani ni ipi? na ni lugha zipi nyingine unazoongea?
Relation status yako? kilichowahi kukufurahisha sana kwenye maisha yako, kilichowahi kukuhuzunisha sana?
ni kitu gani kibaya sana ulishawahi kukifanya? elezea ndani ya maneno 50, zitaje tabia zako zinazokera wengine, wewe ni mdini? eleza msimamo wako wa kisiasa.
Elezea uhusiano wako na mtu uliechagua kuingia nae, eleza kwa nini unataka kuingia BBA, elezea uhusiano wako na familia, elezea aina ya maisha unayoishi, Afya yako, unavuta sigara? kama ndio, ngapi kwa siku?
maswali haya yafuatayo, hayatakufanya ushindwe au uweze kuingia BBA!!!!!! una matatizo sugu ya kiafya? utakubali kupima HIV? una matatizo ya akili?
BBA ya mwaka huu itaanza May ambapo washiriki kutoka nchi 15 za Afrika watashiriki

0 comments:

Post a Comment

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Facebook Themes