KARIBU

Tuesday, February 14, 2012

Mtoto wa sumari ataka kumrithi baba yake

MBIO za kuwania ubunge wa Arumeru Mashariki zimeanza na tayari jana wananchama wawili wa CCM walijitokeza kuchukua fomu kuwania tiketi ya kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Edson Lihweuli amewataja waliochukua fomu zilizoanza kutolewa jana kuwa ni Williamu Sarakikya (38) na Sioi
Sumari.
Kwa mujibu wa Lihweuli, Sarakikya ambaye ni mkazi wa Nkoaranga ndiye aliyekuwa mwanachama wa kwanza kuchukua fomu hiyo na kufuatiwa na Sioi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Akheri. Sioi ni mtoto wa kwanza wa marehemu Sumari; mbunge aliyepita aliyepita katika Jimbo hilo la Arumeru Mashariki.
Tambo za wagombea
Mara baada ya kuchukua fomu, Sarakikya alisema katika uchaguzi uliopita alikosa nafasi hiyo ya kuteuliwa kwa kuwa alikuwa mgenikatika siasa. Sarakikya alisema katika muda huo alijifunza mengi kuhusu siasa na sasa amejipanga kikamilifu kuwania nafasi hiyo na hatafanya makosa.
Naye Sioi alisema amechukua fomu za kuwania ubunge, ili ashiriki kupunguza ama kumaliza changamoto zilizopo ndani ya jimbo hilo. Sumari alisema yeye ni mkazi wa jimbo hilo na ameshatembelea matawi yote na kujua changamoto hizo ila kwa sasa hawezi kuzitaja mpaka muda ukifika atazitaja na namna gani atashirikiana na wana CCM na wasio wana CCM kuzipatia ufumbuzi.
Mgombea wa CCM
Wakati huo huo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) iliyomaliza kikao chake Dodoma juzi, imetoa ratiba ya mchakato wa kumpata mgombea wa chama hicho atakaye peperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi huo.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo ya NEC iliyokuwa ikiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete, mgombea wa chama hicho atatangazwa rasmi Februari 27, mwaka huu na Kamati Kuu ya chama hicho.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema jana kuwa mwisho wa kuzirudisha fomu zilizoanza kutolewa jana ni Februari18, mwaka huu. Alisema Februari 20,mwaka huu Mkutano Mkuu wa jimbo hilo utaitishwa ili kupiga kura za maoni, tofauti na ilivyozoeleka kura hizo kupigwa kwenye matawi.
“Mabadiliko haya ni kwa uchaguzi huu mdogo tu kwa sababu hatuna muda wa kuzunguka kwenye matawi yetu yote ya jimbo hilo,” alisema Nape. Alisema Februari 21, mwaka huu Kamati ya Siasa ya Wilaya itajadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati ya Siasa ya Mkoa na Februari 24 mwaka huu Kamati hiyo ya mkoa itajadili na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu ya CCM.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 27 mwaka huu Kamati Kuu ya chamahicho itateua na kumtangaza rasmi mgombea wa chama hicho katika jimbo hilo. Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Jeremeih Sumari kufariki dunia mapema mwezi uliopita kwa ugonjwa wa saratani ya ubongo.
Uchaguzi wa madiwani
NEC pia ilitoa ratiba ya uchaguzi wa madiwani katika kata nane za Tanzania Bara ambazo pia wanachama walianza kuchukua fomu jana lakini mwisho wa kuzirejesha utakuwa Februari 16, mwaka huu. Nape alisema kuanzia Februari 17 hadi 21, mwaka huu itakuwa ni muda wa kampeni za uchaguzi kwenye matawi hayo na Februari 22 kutafanyika mikutano mikuu ya matawi ya kupiga kura za maoni.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Februari 25 mwaka huu kamati za siasa za wilaya zitajadili wagomea na kutoa mapendekezo yao kwa kamati za siasa za mikoa ambazo nazo zitawajadili wagombea hao na kutoa mapendekezo Februari 27 na halmashauri kuu za mikoa zitateua wagombea Februari 29, mwaka huu.
Taarifa zingine NEC
Pamoja na hayo, Nape alisema NEC pia ilipokea maelezo kutoka serikalini kuhusu kumalizika kwa mgogoro wa madaktari nchini na mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya. “Wajumbe wameitaka Serikali kuhakikisha inachukua hatua haraka za kumaliza kabisa mgogoro huo ili usirejee tena na kuitaka ijijengee utamaduni wa kumaliza migogoro kama hiyo mapema kabla ya kuleta madhara makubwa kwa wananchi,” alisema.
Alisema mkutano huo pia ulijadili suala la chama hicho kuanzisha Kamati ya Maadili ambapo mjadala mkali uliibuka wa kutaka ama kamati hiyo iingizwe kwenye katibaya chama hicho au la.
Alisema katika kukamilisha mambo zaidi ya 20 ya mabadiliko ya chama hicho ikiwemo kujivua gamba, tayariwameanza kupata mafanikio hasa katika eneo la kutaka chama hicho kujiendesha chenyewe bila kutegema ruzuku. Kwa sasa kwa mujibu wa Nape, mikoa mitatu ikwemo Mwanza, Arusha na Dar es Salaam inajiendesha yenyewe

Washindi wa tuzo za grammy

Tuzo za Grammy 2011 zenye Category 78 zimetolewa nchini Marekani usiku wa kuamkia leo ambapo ulikua ni usiku pia wa kumkumbuka Whitney Houston, kabla mzigo hujaanza nataka nikupitishe kwanza kwa baadhi ya picha za waliostua kwenye REDCARPET.
rapper Nicki Minaj akiwa na mtu asiefahamika ambae alivaa kama Papa.
huyu mrembo aliwasili na Adam Levine
Mwimbaji Adele ndio ameongoza kwa waimbaji wa kike waliochukua tuzo nyingi usiku huo ambapo amechukua tuzo sita.
RECORD OF THE YEAR: Rolling In The Deep (ADELE)
ALBUM OF THE YEAR: 21 -(ADELE)
SONG OF THE YEAR: Rolling In The Deep (ADELE)
BEST NEW ARTIST: Bon Iver
BEST POP SOLO PERFOMANCE: Someone Like You (ADELE)
Best Pop Duo/Group Performance: Body And Soul Tony Bennett & Amy Winehouse
Best Pop Vocal Album: 21 (ADELE)
Best Traditional Pop Vocal Album: Duets II Tony Bennett & Various Artists
Best Rock Performance: Walk Foo Fighters
Best Rock Song: Walk Foo Fighters
Best Rock Album: Wasting Light Foo Fighters
Best R&B Performance: Is This Love Corinne Bailey Rae
Best Traditional R&B Performance: Fool For You Cee Lo Green & Melanie Fiona
Best R&B Song: Fool For You Cee Lo Green, Melanie Hallim, Jack Splash, songwriters (Cee Lo Green & Melanie Fiona)
Best R&B Album: F.A.M.E. - Chris Brown
Best Rap Performance: Otis (Jay-Z & Kanye West)
Best Rap/Sung Collaboration: All Of The Lights (Kanye West, Rihanna, Kid Cudi & Fergie)
Best Rap Song: All Of The Lights - (Kanye West, Rihanna, Kid Cudi & Fergie) ambapo zilizokua
zinashindania hiyo tuzo ni Black And Yellow, I Need A Doctor, Look At Me Now, Otis
na The Show Goes On ya Lupe Fiasco.
Best Rap Album: My Beautiful Dark Twisted Fantasy (Kanye West)
Best Country Solo Performance: Mean(Taylor Swift)
Best Country Song: Mean - Taylor Swift, songwriter (Taylor Swift)
Best Gospel/Contemporary Christian Music Performance: Jesus - Le'Andria Johnso
Best Gospel Song: Hello Fear - Kirk Franklin, songwriter (Kirk Franklin)
Best Gospel Album: Hello Fear - Kirk Franklin
Hapo chini ni VIDEO ya Perfomance ya Rihanna kwenye tuzo hizo……
Washindi wengine wa Grammy mwaka huu ni Best American Album: Ramble At The Ryman – Levon Helm
Best Reggae Album: Revelation Pt 1: The Root Of Life - Stephen Marley
Best World Music Album: Tassili - Tinariwen
Best Comedy Album: Hilarious -Louis C.K.
Best Historical Album: Band On The Run - (Paul McCartney Archive Collection - Deluxe Edition)
Paul McCartney, compilation producer; Sam Okell & Steve Rooke, mastering engineers
(Paul McCartney & Wings)
Best Short Form Music Video: Rolling In The Deep -Adele
Producer Of The Year, Non-Classical: Paul Epworth ambae amehusika kutengeneza hits kama
*. Call It What You Want (Foster The People) (T)

Thursday, February 2, 2012

Ajali yaua wanafunzi saba korogwe girls

Vifo hivyo vimetokea baada ya mwanafunzi aitwaye KIBIBI MMASA kuingia ndani ya gari la kaka yake lenye namba T489 AGJ na kuanza kulichezea,wakati akiwa ndani ya gari mara akaweka gia ya kurudi nyuma na kuanza kurudi nyuma kwakasi ya 120 km kwa saa na kuwaparamia wanafunzi waliokuwa katika kusherekea mahafali hayo na kusababisha vifo hivyo.

Fomu za big brother zatoka

Fomu za ushiriki wa shindano la BIG BROTHER AFRICA zimetoka leo, ambapo tayari mpaka saa tano asubuhi watanzania zaidi ya 15 walikua tayari wamejitokeza kuchukua hizo fomu ambazo zinatolewa bure.
haya ni baadhi ya maswali yaliyopo kwenye fomu.
historia yako, lugha ya nyumbani ni ipi? na ni lugha zipi nyingine unazoongea?
Relation status yako? kilichowahi kukufurahisha sana kwenye maisha yako, kilichowahi kukuhuzunisha sana?
ni kitu gani kibaya sana ulishawahi kukifanya? elezea ndani ya maneno 50, zitaje tabia zako zinazokera wengine, wewe ni mdini? eleza msimamo wako wa kisiasa.
Elezea uhusiano wako na mtu uliechagua kuingia nae, eleza kwa nini unataka kuingia BBA, elezea uhusiano wako na familia, elezea aina ya maisha unayoishi, Afya yako, unavuta sigara? kama ndio, ngapi kwa siku?
maswali haya yafuatayo, hayatakufanya ushindwe au uweze kuingia BBA!!!!!! una matatizo sugu ya kiafya? utakubali kupima HIV? una matatizo ya akili?
BBA ya mwaka huu itaanza May ambapo washiriki kutoka nchi 15 za Afrika watashiriki

pata nguo kali kutoka izzo biz clasic wear

wiki hii itakua ni nzuri sana kwa msanii anaeiwakilisha Mbeya, mzee wa kuongea na mshua, Izzo B atazindua duka lake jipya jijini mbeya maeneo ya soweto stand ya kuelekea mjini."duka langu linaitwa
IZZO BIZNESS CLASSIC WEAR alisema Izzo"..Hongera zake za kutosha, keep it locked

boti zagongana mwanza, 30 wafariki

0digg



share

Boti zagongana, 30 wanusurika kifo!

ZAIDI ya watu 30 wamenusurika kufa kwa kuzama majini, baada ya boti walizokuwa wakisafiria kugongana katika Ziwa Victoria, Wilaya ya Musoma Vijijini Mkoani Mara; imethibitishiwa.
Imeelezwa kwamba ajali hiyo imetokea hii leo majira ya saa 3:15 asubuhi katika eneo Rethi, ambapo boti moja iliyokuwa ikisafirisha abiria kutoka Mwigobero mjini Musoma kwenda Kisiwa cha Rukuba kugongana uso kwa uso na boti nyingine ya wavuvi, jambo lililosababisha taharuki kubwa.Taarifa kutoka mjini Musoma zinaeleza kwamba, boti ya abiria ilikuwa na watu 28 na mizigo nyingi, huku boti ya wavuvi ikiwa imebeba wavuvi wawili, na kwamba watu wote waliokolewa.
Kwa mujibu wa taarifa hizo zilizothibitishwa pia na Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Robert Boaz (RPC), zinasema kwamba, baada ya boti hizo kugongana iliharibika na kusababisha maji mengi kuanza kujaa ndani, ambapo abiria wote walipatwa na hofu kubwa.
“Ni kweli ajali ipo na watu kama 30 hivi nusura wafe kwa kuzama majini. Watu hawa walikuwa kwenye boti ndani ya Ziwa Victoria, lakini boti hizo hazikuwa na vifaa vya kujiokolea.
“Hii ajali imetokea asubuhi leo, na abiri walikanyagana baada ya ajali kutokea. Kila mmoja alitaka ajiokoe mwenyewe kabla ya kuokolewa”, alisema mashuhuda mmoja wa ajali hiyo, Fikiri Aloyce Malenge.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoani Mara, Robert Boaz alisema: “Kweli hii ajali imetokea leo, majira ya saa 3 hivi asubuhi. Na katika ajali hii boti moja ilikuwa na abiria 28, lakini ile ya wavuvi ilikuwa na watu wawili?
“Hizi boti ya wavuvi na ile ya abiria zimegongana uso kwa uso. Lakini watu wote walifanikiwa kuhamia kwenye boti ya wavuvi na hakuna aliyefariki dunia hata mmoja”, alisema Kamanda wa Polisi Mkoa huo wa Mara, Boaz.
Alisema, chanzo cha ajali bado hakijajulikana na kwamba jeshi lake linaendelea na uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo mbaya, na kwamba hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo?
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Boaz, abiria wote walipatiwa huduma ya kwanza papo hapo na kuruhusiwa kuendelea na majukumu yao ya kawaida.
Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – Mwanza

mkenya aingia uchi uwanjani

Jamaa mmoja mwenye asili ya kenya aliingia uwanjani akiwa uchi wa mnyama kwenye mechi kati ya England na Argentina kwenye michuano ya Rugby World Cup - 2011 inayofanyika nchini New Zealand .

Inasemekana jamaa ni mzaliwa wa Kenya ana miaka 23 na alikua hajavaa kitu zaidi ya kuchora uso wake,na alikatiza kwenye uwanja wa Otago na kuonekana na mamilioni ya watazamaji wa television duniani,baadaye alikamatwa na wana usalama na huenda akakabiliwa na kifungo che miezi 3 jela au faini ya dola 5,000.
Wachambuzi wa mambo wanadai kuwa jamaa huyo aliamua kufanya hivyo ili kujizolea umaaru duniani.

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Facebook Themes